MHE. DKT. MASHINJI: UWEPO WA FARU UMECHANGIA IDADI YA WAGENI KUONGEZEKA HIFADHI YA TAIFA SERENGETI Na. Brigitha Kimario - Serengeti Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Vincent Mashinji amesema uwepo wa wanyama Faru katika Hifadhi ya Taifa Serengeti umechangia kuongezeka kwa idadi ya watalii. Ongezeko la wanyama hao ambao ni kivutio kwa watalii wa ndani na nje limechangiwa na juhudi kubwa za ulinzi zinazofanywa na maafisa na askari wa TANAPA waliojitolea kwa jasho na damu kuhakikisha wanyama hawa adimu wanaendelea kuwepo. Dkt. Mashinji ameyasema hayo leo tarehe 22.09.2023 ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Faru duniani yaliyofanyika Fort Ikoma wilayani Serengeti kwa kushiriki mbio fupi kwa ajili ya kuadhimisha siku hii. Na kusema, "nimefurahi kuambiwa kuwa wanyama hawa adimu idadi yao inaongezeka mwaka hadi mwaka, ongezeko la wanyama hawa limeendelea kuvuta watalii wengi sana wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Niwahakikishie kama Mkuu wa wilaya hii ya Serenge...
Posts
Showing posts from September, 2023