KUNDI LINGINE LA WANANCHI 541 LAHAMA NGORONGORO

KUNDI LINGINE LA WANANCHI 541 LAHAMA NGORONGORO Na Mwandishi wetu, NCAA. Hamasa ya wananchi wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro imeongezeka ambapo leo tarehe 19 February , 2024 jumla ya kaya 82 zenye wananchi 541 na mifugo 3,379 zimehama kutoka Ngorongoro kweda Kijiji cha Msomera Handeni Tanga. Akizungumza wakati wa kuaga kundi hilo Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Richard Kiiza amesema kuwa baada ya kuhama kwa kundi hilo leo inafanya idadi ya wananchi waliokwishahama ndani ya hifadhi tangu zoezi lilipoanza hadi leo kufikia kaya 1,032 zenye watu 6,395 na mifugo 28,982. Kamishna Kiiza amebainisha kuwa kadri siku zinavyoenda wananchi wengi wanahamasika na kujiandikisha kuhama kwa hiari yao wenyewe hasa baada ya ushuhuda wa maisha mazuri kwa wananchi wenzao waliokwishatangulia ambao Maisha yao yamebadilika kwa kiasi kikubwa. “Wananchi waliotangulia mwaka jana wengi wao wamejenga nyumba za kisasa, wamelima mazao ya kutosha kwa ajili ya chakula na ...