KAMISHNA KUJI: AHIMIZA WATUMISHI KUJIENDELEZA KIELIMU ILI KUBORESHA UFANISI KATIKA UTENDAJI
Na. Philipo Hassan - Arusha Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), CPA Musa Nassoro Kuji, amewataka Maafisa na Askari Uhifadhi wa Uhifadhi waliopo TANAPA Makao Makuu na Kanda ya Kaskazini kujiendeleza kielimu ili kuboresha ufanisi katika utendaji kazi. Aliyasema hayo leo Julai 16, 2025, alipofanya kikao kazi cha Maafisa na Askari waliopo TANAPA Makao Makuu na Kanda ya Kaskazini, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kibo uliopo katika eneo la Makao Makuu ya TANAPA katika Jengo la Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jijini Arusha. Akizungumza katika kikao hicho, Kamishna Kuji alieleza umuhimu wa kujiendeleza kielimu, jambo ambalo linasaidia kuongeza ujuzi, maarifa ya kukabiliana na changamoto zinapojitokeza, kuboresha huduma nyakati za kuwahudumia watalii na kuwa wabunifu ili kuleta ufanisi mahali pa kazi. “Katika utendaji wenu wa kila siku kama watumishi wa TANAPA, tunategemea sana maarifa na weledi wenu ili kuboresha utendaji kazi. Hivyo, k...