MWAROBAINI WA MIUNDOMBINU KOROFI SERENGETI WAPATIKANA

MWAROBAINI WA MIUNDOMBINU KOROFI SERENGETI WAPATIKANA Na. Edmund Salaho/Serengeti. Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA Juma Kuji leo amefanya ziara ya kukagua miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti na kuiagiza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kushughulikia mara moja maeneo korofi ya barabara ndani ya hifadhi hiyo, ili watalii wafikie adhma yao ya kutembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti. Akizungumza baada ya kukagua maeneo hayo Kamishna Kuji, ameielekeza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kurekebisha maeneo yote korofi na kuhakikisha kuwa hakuna maeneo ambayo hayatapitika licha ya uwepo wa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ili kupunguza adha kwa wageni. “Licha ya changamoto ya mvua kubwa zinazoendelea hatuwezi kusubiri ziishe tumeazimia kushughulikia kwa haraka maeneo yote korofi ikiwa ni hatua za haraka, lakini lengo kuu ni kuhakikisha barabara hizi zinakuwa na tabaka gumu, haya ni maagizo yangu kwa menejimenti kuhakikisha barabara zote zi...