MAKAMU WA RAIS WA CUBA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valdés Mesa amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 23 - 25 Januari, 2024. 

Mara baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Mesa alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)

Akiwa nchini, Mhe. Mesa atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete na pia atatembelea taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Mhe. Mesa pia atamtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere pamoja na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa za viuadudu ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.








Comments

Popular posts from this blog

KUNDI LINGINE LA WANANCHI 541 LAHAMA NGORONGORO

𝐔𝐉𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 “𝐒𝐄𝐑𝐄𝐍𝐆𝐄𝐓𝐈 𝐍𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍𝐀𝐋 𝐏𝐀𝐑𝐊 𝐆𝐎𝐋𝐅 𝐂𝐎𝐔𝐑𝐒𝐄” 𝐖𝐀𝐅𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟒𝟐

UTALII WA MALIKALE WASHIKA KASI NCHINI, WAFARANSA WAFURIKA KILWA KISIWANI