๐๐๐๐๐๐ ๐๐ โ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐โ ๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐
* ๐ข๐๐๐๐๐ถ๐โ๐ ๐ฏ๐๐ถ๐ ๐๐ถ ๐ฟ๐๐๐ถ๐๐ ๐๐ถ๐๐พ๐ ๐พ๐๐ถ ๐๐๐ถ ๐๐ถ๐๐ถ ๐๐ถ ๐๐๐ถ๐๐๐ถ ๐ฎ๐๐๐๐๐๐๐๐พ.
Na. Catherine Mbena, SERENGETI.
Ujenzi wa mradi wa kimkakati wa uwanja wa gofu Hifadhi ya Taifa Serengeti โSerengeti National Park Golf Courseโ uliobuniwa na Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania chini ya Mwenyekiti wake Jenerali (Mstaafu) George Waitara unaojengwa katika eneo la Fort Ikoma, nje kidogo ya Hifadhi ya Taifa Serengeti umefikia asilimia 42.
Utekelezaji huo unajumuisha ujenzi wa โTee and Greenโ kwa mashimo kumi na nane; mashimo tisa ya kwanza (front- nine/inbound holes), mashimo tisa ya nyuma (back - nine/outbound holes), uchimbaji wa visima virefu viwili vyenye uwezo wa kutoa maji kiasi cha lita elfu kumi kwa saa kwa kila moja, uchimbaji na ujenzi wa mabwawa ya maji mawili yenye ujazo wa takribani lita millioni 22 kila moja, ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 5.2 kuzunguka uwanja mzima, ujenzi wa โpower houseโ na ufungaji wa pampu za maji pamoja na โ solar panels โ kwenye visima viwili vilivyochimbwa.
Msimamizi wa mradi huu, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Mhandisi Mshauri, Dkt. Richard Matolo alieleza upekee wa uwanja huu kuwa ni pamoja na kuongezwa urefu kwa kila shimo (unaojumuisha โTee Fairwayโ na โGreenโ ), hivyo kuufanya uwanja huu kuwa moja ya viwanja virefu duniani, kupindishwa kwa baadhi ya mashimo โdog leggingโ na uwepo wa miti kwenye baadhi ya mashimo na hivyo kuwa changamoto kubwa kwa mchezaji.
โNi uwanja wa kipekee ukilinganisha na viwanja vingine vya gofu duniani. Upekee wa uwanja huu siyo tu kwa sababu unajengwa kwenye eneo la hifadhi maarufu duniani ya Serengeti, bali pia unatokana na sifa za makusudi zilizoongezwa kwenye usanifu wake. Ni watu wachache sana ambao ni wachezaji bingwa wa gofu watakaoweza kucheza na kumaliza ndani ya vigezo vinavyotambulika kimataifa.โ aliema Dkt. Matolo.
Wakizungumza mara baada ya kucheza kwa mara ya kwanza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara katika uwanja huo. Mhe. Balozi Charles Sanga, Mhe. Balozi Job Masima na Mhe. Dkt. Edmund Mndolwa walifurahi kucheza katika uwanja huo kwa mara ya kwanza.
Naye, Balozi Mhe. Job Masima alisema โUwanja huu ni Game Changer, hakuna uwanja utaenda duniani ukakuta ni mkubwa kiasi hiki wenye mandari nzuri na wanyama.
Aidha, Balozi Charles Sanga alieleza kuwa โIle ndoto yetu ya kuwa na uwanja wa kisasa wa Gofu Serengeti tunaona inaenda kutimia na maendeleo ya ujenzi wa uwanja huu ni mazuri sanaโ.
Mradi huu unatoekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 450 utagharimu kiasi cha shilingi bilioni tisa na nusu unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025.
Comments