Posts

Showing posts from February, 2025

RAIS DKT. SAMIA: BARABARA MPYA YA TANGA, PANGANI, SAADANI NA BAGAMOYO KUIFUNGUA TANGA KIUTALII

Image
Na Philipo Hassan - Tanga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema kuwa kukamilika kwa barabara ya lami inayounganisha Tanga, Pangani, Saadani na Bagamoyo pamoja na Daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525 zitasaidia kuifungua Tanga Kiutalii na kiuchumi. Rais Samia ameyasema hayo leo, Februari 26, 2025 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa  barabara na Daraja la Mto Pangani ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake mkoani Tanga. Vilevile, alisisitiza kuwa miundombinu hiyo mipya itarahisisha maeneo mengi ya utalii kufikika kiurahisi. Rais Samia alieleza “Barabara hii tunayoiunganisha inaenda kuifungua Tanga kiutalii na kibiashara. Maeneo mbalimbali ya kiutalii ambayo hayafikiki, itakuwa ni rahisi kumtoa mtalii Hifadhi ya Taifa Saadani na kwenda kutalii maeneo mengine ndani ya Mkoa wa Tanga”  Naye, Mbunge wa jimbo la Pangani Mhe. Jumaa Aweso alimshukuru Rais Samia kwa kutekeleza mradi mkubwa wa barabara na Daraja ambayo yat...

SIX RIVER AFRICA NA ECO WASHIRIKIANA NA TANAPA KUBORESHA HUDUMA ZA MATIBABU YA WANYAMAPORI

Image
Na. Happiness Sam- Same Shirika la Six Rivers Africa pamoja na Elephant Conservation Organisation (ECO) yameungana na TANAPA ili kuimarisha huduma za matibabu ya wanyamapori katika hifadhi za kanda ya kaskazini kwa kuongeza vitendea kazi ikiwemo gari, vifaa tiba pamoja na dawa za kutibu wanyamapori ili kuhakikisha ustawi wa wanyamapori unaimarika katika maeneo hayo. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Tiba ya Wanyamapori, jana Februari 18, 2025 katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi iliyopo Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro, Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni alieleza umuhimu wa uhifadhi kwa maendeleo ya taifa kwani unasaidia katika kutunza urithi wetu wa asili ikiwemo wanyamapori kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo. DC Mgeni alisema  “Mradi wa Tiba ya Wanyamapori (Veterinary Support Project) ulianzishwa mwaka 2013 katika Hifadhi yetu ya Taifa ya Mkomazi kwa lengo la kuchukua hatua muhimu katika kuhakikisha mafanikio endelevu ya juhudi zetu za uhifadhi, mradi ...

WAZIRI CHANA AFUNGUA RAS ONESHO LA WIKI YA UBUNIFU LA ITALIA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
• Aipongeza Italia kwa mashirikiano katika sekta ya utalii Na Happiness Shayo- Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amefungua rasmi Onesho la Wiki ya Wabunifu wa Italia linaloonesha picha za wabunifu mbalimbali wakubwa wa zamani kutoka nchini Italia na  kuipongeza nchi hiyo kwa ushirikiano kati yake na Tanzania kwenye sekta ya utalii. Ufunguzi huo umefanyika  leo Februari 10,2025 katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Jijini Dar es Salaam ambapo onesho hilo linatarajiwa  kumalizika Februari 20,2025 likiwa na lengo la kukuza ushirikiano katika masuala ya utalii, historia na uchumi.  “ Italia imejitolea katika juhudi zetu za kukuza utalii endelevu na kuhifadhi urithi wetu wa asili na kiutamaduni .Mfano mmoja mzuri wa ushirikiano huu ni mradi wa Kisiwa cha Bawe, ambao ni mwanzo mzuri unaoonyesha utalii endelevu. Mradi huu hauangazii tu uzuri wa visiwa vya Tanzania bali pia unaonesha matokeo chanya ya uwekezaji wa ki...