RAIS DKT. SAMIA: BARABARA MPYA YA TANGA, PANGANI, SAADANI NA BAGAMOYO KUIFUNGUA TANGA KIUTALII
Na Philipo Hassan - Tanga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema kuwa kukamilika kwa barabara ya lami inayounganisha Tanga, Pangani, Saadani na Bagamoyo pamoja na Daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525 zitasaidia kuifungua Tanga Kiutalii na kiuchumi. Rais Samia ameyasema hayo leo, Februari 26, 2025 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara na Daraja la Mto Pangani ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake mkoani Tanga. Vilevile, alisisitiza kuwa miundombinu hiyo mipya itarahisisha maeneo mengi ya utalii kufikika kiurahisi. Rais Samia alieleza โBarabara hii tunayoiunganisha inaenda kuifungua Tanga kiutalii na kibiashara. Maeneo mbalimbali ya kiutalii ambayo hayafikiki, itakuwa ni rahisi kumtoa mtalii Hifadhi ya Taifa Saadani na kwenda kutalii maeneo mengine ndani ya Mkoa wa Tangaโ Naye, Mbunge wa jimbo la Pangani Mhe. Jumaa Aweso alimshukuru Rais Samia kwa kutekeleza mradi mkubwa wa barabara na Daraja ambayo yat...