KAMPENI YA TWENZETU KILELENI 2024 YAWAVUTA WAMAREKANI


Na. Happiness Sam- Kilimanjaro 

Wakati pazia la Twenzetu Kileleni msimu wa nne likiwa limefunguliwa rasmi leo Disemba 03, 2024 katika Lango la Lemosho lililopo wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro, limevutia pia watalii kutoka Taifa la Marekani ambao wameungana na Watanzania wapatao 33 kwenda katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika ifikapo tarehe 09.12.2024.

Akiwaaga wapandaji hao Mhe.Dkt Christopher David Timbuka Mkuu wa Wilaya ya Siha alisema, "Nimefarijika kuona idadi ya wapandaji imeongezeka kutoka watalii 11 waliopanda mwaka 2023 na kufikia wapandaji 33 mwaka huu 2024 ambapo idadi hii ni zaidi ya asilimia 100% huku zoezi hilo likiendelea kujizolea umaarufu na kuvuka mipaka ya Tanzania na kwenda mbali zaidi  kuvutia watalii kutoka Taifa la Marekani.โ€


Mhe. Dkt.Timbuka pia alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya African Scenic kwa kuipa hadhi njia ya Lemosho kuwa ni miongoni mwa njia inayotumika mwezi Disemba katika zoezi la kupandisha watu wa mataifa mbalimbali kuadhimisha uhuru wa Tanganyika .p

Akimkaribisha mgeni rasmi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Kanda ya Kaskazini Betrita Lyimo alisema mbali na kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika, kampeni hii ya TWENZETU KILELENI ina mchango mkubwa wa kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hii.

Aidha, Kamishna Betrita Lyimo aliongeza kuwa ujio wa wapanda Mlima hawa kila mwaka wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato na mkoa na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kutokana na bidhaa mbalimbali wanazonunua katika zoezi zima la kupanda mlima huo.

Naye, Mkurugenzi wa African Scenic Simbo Natai alisema kuwa mbali na kuwashukuru TANAPA kuwapa ridhaa ya kutumia njia ya Lemosho katika Kumbukizi ya Uhuru wa Tanganyika pia ameahidi kuitangaza njia hiyo katika mataifa mbalimbali ili kupata watalii wengi watakoungana na watanzania nyakati za Disemba kusherehekea sikukuu za Uhuru katika kilele hicho.

Ndg.John Pangilinan ambaye ni miongoni mwa raia wa Marekani walioshiriki kupanda Mlima Kilimanjaro alisema kuwa alipata shauku na hamasa ya kupanda mlima huo kutokana na matangazo mbalimbali ya TWENZETU KILELENI aliyoyaona katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kwenye Website ya TANAPA.

Kampeni ya "Twenzetu Kileleni " 2024  yenye lengo la kupandisha Watanzania kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 63 ya uhuru  wa Tanganyika imebeba dhima ya kizalendo, umoja na mshikamano tulioachiwa na waasisi wa Taifa hili.











Comments

Popular posts from this blog

KUNDI LINGINE LA WANANCHI 541 LAHAMA NGORONGORO

๐”๐‰๐„๐๐™๐ˆ ๐–๐€ โ€œ๐’๐„๐‘๐„๐๐†๐„๐“๐ˆ ๐๐€๐“๐ˆ๐Ž๐๐€๐‹ ๐๐€๐‘๐Š ๐†๐Ž๐‹๐… ๐‚๐Ž๐”๐‘๐’๐„โ€ ๐–๐€๐…๐ˆ๐Š๐ˆ๐€ ๐€๐’๐ˆ๐‹๐ˆ๐Œ๐ˆ๐€ ๐Ÿ’๐Ÿ

UTALII WA MALIKALE WASHIKA KASI NCHINI, WAFARANSA WAFURIKA KILWA KISIWANI